ODUOR AWAONDOA WACHEZAJI 12 KIKOSI CHA STARLETS
Kocha wa muda wa Harambee Starlets Geoffrey ‘Solo’ Oduor amefanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha wachezaji 29 kitakachocheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Tanzania mwezi ujao, akiwaacha nje wachezaji 12 waliowakilisha Kenya katika mashindano ya WAFCON 2026 nchini Morocco.
Miongoni mwa walioachwa ni beki Elizabeth Ochaka pamoja na washambuliaji Mercy Airo na Violet Nanjala, huku Oduor akilenga kukijenga upya kikosi baada ya Kenya kupoteza mechi zote tatu za makundi bila kufunga bao.
Starlets itakabiliana na Tanzania Desemba mosi na nne, mechi zitakazompa kocha nafasi ya kutathmini kikosi kipya na kuandaa mchanganyiko wa wachezaji kwa mashindano yajayo ya kimataifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

