OKOTH OBADO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 25 JELA
Aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado amehukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani kwa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno, Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Cecilia Wairimu Githua katika Mahakama za Milimani jijini Nairobi.
Katika hukumu hiyo aliyekuwa msaidizi wa kibinafsi wa Obado, Michael Juma Oyamo pia amehukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani kwa kuhusika katika mauaji hayo.
Hata hivyo, aliyekuwa Karani wa Kaunti ya Migori, Caspal Ajwang Obiero, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani kuhusiana na mauaji ya Sharon Otieno.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo

