Friday, November 27, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

SERIKALI YAPANGA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 5.2 KWA MWAKA UJAO

Hazina ya Kitaifa imependekeza bajeti ya shilingi trilioni 5.235 kwa mwaka wa fedha wa 2027/2028, ikiwa ni ongezeko kutoka trilioni 4.819 katika mwaka huu wa fedha, Waziri wa Hazina John Mbadi akiwasilisha mapendekezo hayo mbele ya kamati ya Seneti kuhusu fedha na bajeti.

Serikali inalenga kukusanya mapato ya trilioni 3.923 dhidi ya matumizi ya trilioni 5.235, huku matumizi ya kawaida yakikadiriwa kuwa trilioni 3.88 na miradi ya maendeleo ikitengewa shilingi bilioni 917.

Upungufu wa fedha unakadiriwa kufikia takriban trilioni 1.2, utakaofadhiliwa kupitia mikopo ya nje na ya ndani, huku Hazina ikionya kuwa gharama za deni la taifa na shinikizo la matumizi vinaendelea kupunguza nafasi ya serikali kugharamia huduma na miradi mingine.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *