GACHAGUA ATOA WITO WA UMOJA KWA JAMII ZA KIKUYU NA WASOMALI
Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua amezitaka jamii za Kikuyu na Wasomali zinazoishi na kufanya biashara eneo la Eastleigh jijini Nairobi kukataa siasa za migawanyiko na kudumisha ushirikiano wao wa muda mrefu.
Akihutubia mikutano ya hadhara akiwa na viongozi wengine wa DCP, Gachagua alidai kuwa baadhi ya wanasiasa wanatumiwa na serikali kuchochea uhasama kati ya jamii hizo, akizitaka kuendelea kushirikiana katika biashara na siasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

