Friday, November 27, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

EACC YATAKA VYOMBO VYA HABARI KUCHUNGUZA WAGOMBEA WA 2027

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC, imevitaka vyombo vya habari kuchunguza kwa kina watu wanaowania nyadhifa za uongozi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, ili kuwasaidia Wakenya kufanya maamuzi yanayozingatia uadilifu na uwajibikaji.

Akizungumza mjini Mombasa katika mkutano wa EACC na Chama cha Wahariri nchini, mwenyekiti wa tume hiyo David Oginde amesema wanahabari hawapaswi kuvutiwa na miungano ya kisiasa au ahadi za kampeni pekee, bali wachunguze pia tabia, sifa za kitaaluma na rekodi za wagombea.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *