Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

JKUAT COUGARS YAJIANDAA KWA KENYA CUP

Kocha wa JKUAT Cougars, Smith Muhoya, amesema timu yake iko tayari kwa kampeni yake ya kwanza katika ligi kuu ya raga ya Kenya Cup, itakapoikaribisha Nakuru RFC katika uwanja wa JKUAT.

Muhoya amesema timu ilifanya maandalizi mazuri ya kabla ya msimu, licha ya kushindwa kutetea taji la mashindano ya Floodlit. Cougars pia ilitumia wiki mbili kutembelea uwanja wa mazoezi wa KCB Ruaraka ili kuzoea ushindani wa kiwango cha juu

Cougars ilipandishwa daraja baada ya kuishinda Homeboyz kwa alama 40-9 katika nusu fainali ya KRU Championship, kabla ya kushindwa na Mwamba RFC kwa alama 34-33 katika fainali na kumaliza ya pili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *