GACHAGUA ADAI VITAMBULISHO VINACHELEWA KUTOLEWA
Kiongozi wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, ameituhumu Idara ya Usajili wa Watu kwa kuchelewesha kwa makusudi utoaji wa vitambulisho vya taifa kwa vijana katika maeneo yanayochukuliwa kuwa ngome za upinzani.
Gachagua amedai kuwa maombi ya vitambulisho katika maeneo yanayounga mkono serikali hushughulikiwa ndani ya siku chache, huku yale ya maeneo ya upinzani yakichukua hadi miezi sita au saba.
Aidha, amesisitiza kuwa DCP itasimamisha wagombea katika nafasi zote za kuchaguliwa, badala ya kuachia nafasi hizo kwa vyama washirika ndani ya muungano mpana wa upinzani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

