MOTO WATEKETEZA BIASHARA ENEO LA GATAKA RONGAI
Wafanyabiashara katika eneo la Gataka, Rongai wanahesabu hasara baada ya moto mkubwa kuzuka na kuteketeza mali katika majengo yaliyo mkabala na Duka kuu la Destiny mwendo wa saa kumi asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, moto huo unashukiwa kusababishwa na mlipuko wa gesi, ingawa chanzo kamili bado hakijathibitishwa.
Maafisa wa zimamoto walifika eneo la tukio kujaribu kudhibiti moto huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha mkasa huo na kiwango cha hasara iliyosababishwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

