CHUO KIKUU CHA MOI KUANZA MPANGO WA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI
Chuo Kikuu cha Moi kinatarajia kuanza mpango mkubwa wa mageuzi utakaohusisha kupunguza idadi ya wafanyakazi, katika juhudi za kukinusuru kutokana na changamoto za kifedha zilizodumu kwa zaidi ya muongo mmoja.
Kaimu Naibu Chansella, Profesa Kiplagat Kotut, ameiambia Kamati ya Bunge ya Elimu kuwa chuo kinafanya tathmini ya majukumu ya wafanyakazi ili kubaini nafasi zitakazoathiriwa na mpango huo.
Hata hivyo, uongozi wa chuo unasema taasisi hiyo, ambayo ilikuwa ikikabiliwa na hatari ya kufilisika, imeanza kuonyesha dalili za kuimarika kufuatia hatua mbalimbali zilizochukuliwa kuirejesha katika hali ya kifedha iliyo bora.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

