Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

NPS: HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA

Msemaji wa Huduma ya Taifa ya Polisi, Michael Muchiri, amesema Inspekta Jenerali wa Polisi ameahidi kuongoza mapambano dhidi ya uhalifu bila ubaguzi.

Muchiri amesema yeyote atakayehusika na vitendo vya uhalifu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, bila kujali cheo au nafasi yake katika jamii.

Kuhusu mbunge anayetajwa katika uchunguzi unaoendelea wa vurugu zilizotokea katika eneo la Keumbu kaunti ya Kisii, Muchiri amesema Mbunge huyo anapaswa kupewa nafasi ya kujibu tuhuma zinazomkabili huku akiwataka wananchi kuziachia mamlaka za uchunguzi kufanya kazi yao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *