IMPALA RFC YAONGEZA MAKOCHA KABLA YA MSIMU MPYA
Mabingwa mara kumi wa Kenya Cup, Impala RFC, wameimarisha benchi lao la ufundi kwa kumteua Michael Kimemia kuwa kocha wa ujuzi na Steve Juma kuwa kocha wa safu ya mbele, kabla ya msimu wa 2026/27 kuanza Jumamosi.
Kocha mkuu Malik Ndemi amesema Kimemia atasaidia kuboresha ujuzi wa msingi wa wachezaji, huku Juma, ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo, akitarajiwa kuimarisha safu ya mbele na maandalizi ya mipira ya kuanzisha mchezo.
Impala walipitia msimu mgumu uliopita, wakishinda mechi tatu pekee kati ya 11 na kumaliza nafasi ya kumi kwa pointi 16, huku Ndemi akisema wameipa kipaumbele safu ya ulinzi baada ya kufungwa majaribio mengi, changamoto iliyojitokeza pia katika mashindano ya Impala Floodlit.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

