BABU OWINO ADAI KUKATAA NAFASI YA WAZIRI WA ELIMU 2024
Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, amedai Rais William Ruto alimpa nafasi ya Waziri wa Elimu wakati wa maandamano ya Gen Z mwaka 2024, lakini akaikataa kutokana na misimamo yake ya kisiasa.
Owino amesema ofa hiyo ilitolewa wakati serikali ilipokuwa ikikabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na maandamano yaliyosababisha Ruto kuvunja Baraza la Mawaziri mwezi Julai mwaka huo.
Amesema alipinga serikali ya upana wa kisiasa na kukataa kujiunga nayo hata baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu marehemu Raila Odinga kuunga mkono mpango huo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

