Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RAIS RUTO AENDELEA KUTETEA UONGOZI WAKE

Rais William Ruto ametetea mageuzi makubwa yanayotekelezwa na serikali yake, akisema Kenya inaweza kufikia maendeleo ya kweli kupitia uongozi thabiti na wenye ujasiri, licha ya ukosoaji wa umma, maandamano na changamoto za kisheria.

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi alipowakaribisha wachezaji na viongozi wa AFC Leopards, Rais Ruto amesema serikali yake imeendelea kusimamia ajenda ya mageuzi kwa uthabiti, akisisitiza kuwa mabadiliko ya kudumu yanahitaji viongozi walio tayari kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya taifa.

Aidha Rais amekariri kuwa kenya  ina uwezo wa kubadilisha uchumi wake kama ilivyofanywa na mataifa mengine yaliyopiga hatua za maendeleo kupitia utekelezaji wa sera na mageuzi ya muda mrefu.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *