Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

EACC YAIDHINISHA SIKU YA KUPAMBANA NA UFISADI NCHINI

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC  inaadhimisha Siku ya Afrika ya Kupambana na Ufisadi kwa kuhimiza kuimarishwa kwa uadilifu, uwajibikaji na uwazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Tume hiyo imesema maadhimisho hayo yanatoa fursa ya kutathmini hatua zilizopigwa katika vita dhidi ya ufisadi na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za umma, sekta binafsi na wananchi katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa.

EACC imeeleza kuwa kuzingatia misingi ya uadilifu na uwajibikaji ni muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za umma, kuimarisha utawala bora na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *