RAIS RUTO ATIA SAINI KUWA SHERIA MISWADA YA KUIMARISHA SEKTA YA FEDHA
Rais William Ruto ametia saini kuwa sheria miswada miwili inayolenga kuimarisha sekta ya fedha nchini na kufanya marekebisho mfumo wa malipo ya kustahafu ya wabunge ili kuendana na katiba na sheria za sasa.
Miswada iliyopitishwa inajumuisha marekebisho ya sheria ya benki kuu CBK na sheria ya marekebisho ya malipo ya kustahafu ya wabunge ambayo imeidhinishwa katika hafla iliyofanyika kwenye ikulu na kuudhuriwa na viongozi wa serikali pamoja na wabunge.
Kupitia sheria mpya CBK itaendelea kuwa na mamlaka ya kutoa msaada wa kifadha kwa taasisi za kifedha zinazokumbwa na changamoto kwa muda.
Samueli Mulu ni karani wa bunge La kitaifa.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

