RUTO AJIBU GACHAGUA KUHUSIANA NA KURA ZA MLIMA KENYA
Rais William Ruto amemjibu aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhusu madai kuwa ndiye aliyemhakikishia kura za Mlima Kenya katika uchaguzi uliopita.
Akizungumza Kaunti ya Embu, Rais amesema alipata uungwaji mkono kwa kufanya kampeni na kuwashawishi wananchi, akiongeza kuwa atarejea katika kaunti zote za Mlima Kenya kuomba muhula wa pili kwa kuzingatia rekodi ya maendeleo ya serikali yake.
Aidha, Rais amewaonya viongozi wa upinzani dhidi ya siasa za ukabila, akiwatuhumu kwa kujaribu kugawanya taifa kwa misingi ya kikabila.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

