JUNIOR STARLETS YAKARIBIA KOMBE LA DUNIA
Timu ya Kenya ya wasichana chini ya miaka 17, Junior Starlets, imekaribia kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuichapa Afrika Kusini mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya mwisho ya kufuzu.
Faith Boke aliifungia Kenya bao la kwanza dakika ya 23, huku kipa Mitchell Okoyo akiokoa penalti muhimu kabla ya Brenda Achieng kuongeza bao la pili dakika ya 70.
Ushindi huo unaipa Kenya nafasi nzuri kuelekea mechi ya marudiano itakayochezwa katika Uwanja wa Nyayo Jumapili, Julai 12.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

