RAIS RUTO AMKARIBISHA RAIS WA ZIMBABWE NCHINI
Rais William Ruto amemkaribisha Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Kenya na Zimbabwe katika sekta mbalimbali za maendeleo na biashara.
Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya pande mbili pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kikanda na bara la Afrika.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo

