Friday, November 27, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

NAIROBI CITY THUNDER YAAGA MASHINDANO YA ROAD TO BAL

Mabingwa mara tatu wa Kenya, Nairobi City Thunder, wameaga mashindano ya kufuzu kwa Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika ya BAL baada ya kuchapwa na Patriots BC ya Sudan Kusini kwa vikapu 83 dhidi ya 75 katika uwanja wa Kasarani Alhamisi usiku.

Thunder ilihitaji ushindi katika mechi hiyo ya mwisho ya Kundi A ili kusalia na matumaini ya kufuzu kwa hatua ya nusu fainali, lakini kichapo hicho kiliwaacha na rekodi ya ushindi mmoja na kushindwa mara mbili.

Patriots BC ilifuzu ikiwa haijapoteza mechi yoyote, ikiungana na Munali Suns ya Zambia, Dar City ya Tanzania na Namuwongo Blazers ya Uganda katika hatua ya nusu fainali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *