MURKOMEN AAGIZA MSAKO DHIDI YA WAHUNI
Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema vyombo vya usalama vinaendelea kuchukua hatua za kukomesha matumizi ya wahuni na vurugu za kisiasa nchini.
Akizungumza katika eneo la Lokori, Kaunti ya Turkana, Murkomen amesema watu 20 wamekamatwa kuhusiana na matukio ya vurugu yaliyotokea Kisumu na Nyahururu siku ya Jumapili.
Aidha, amesema amemwagiza Inspekta Jenerali wa Polisi kuimarisha operesheni dhidi ya wahuni na wafadhili wao bila kujali misimamo yao ya kisiasa au hadhi waliyonayo katika jamii.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

