WACHINA 18 WAKAMATWA KILIMANI KWA TUHUMA ZA ULAGHAI WA MTANDAONI
Raia 18 wa China wamekamatwa jijini Nairobi kufuatia operesheni ya polisi dhidi ya genge linaloshukiwa kujihusisha na ulaghai wa mtandaoni katika eneo la Kilimani.
Operesheni hiyo iliongozwa na maafisa wa DCI kwa ushirikiano na maafisa kutoka Ubalozi wa China, baada ya kupokea taarifa za kijasusi.
Uchunguzi wa awali unaonyesha washukiwa hao walikuwa wakilenga akaunti za watu walioko nje ya nchi na kuelekeza fedha kupitia Kenya kabla ya kuzitoa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

