Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

DUALE ATAKA USHIRIKIANO WA KUPAMBANA NA DAWA BANDIA

Waziri wa Afya Aden Duale ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana katika vita dhidi ya dawa na bidhaa za matibabu zisizo na viwango na bandia ambazo zinaendelea kusambazwa sokoni na kuhatarisha afya ya wananchi.

Duale amesema mbinu ya ushirikiano kati ya sekta mbalimbali itaimarisha juhudi za kukabiliana na mitandao ya kihalifu inayojihusisha na utengenezaji, uagizaji na usambazaji wa dawa hizo.

Amesisitiza kuwa serikali imejizatiti kulinda afya ya wananchi kwa kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria na bidhaa zisizo salama zinaondolewa sokoni.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *