Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

BUNGE LA MACHAKOS LAKABILIWA NA HATARI YA KUFUNGWA

Bunge la kaunti ya Machakos linakaribia kufungwa baada ya wawakilishi wadi kutoa tahadhari kuhusu kushindwa kwa serikali kutoa fedha za kuendesha shughuli tangu mwezi  aprili 2026.

Wakati wa kikao kilichoshuhudia ghadhabu kiongozi wa wachache francis kavyu ameonya kuwa uwezo wa bunge kutekeleza jukumu lake la kikatiba la usimamizi na uwakilishi unapungua kutokana na ukosefu wa rasilimali za kimsingi.

Hata hivyo spika ann kiusya amethibitisha kuwa bunge limewasilisha ombi rasmi kwa kamati ya seneti ili kuingilia kati.

Imetayarishwa na Jones Koikai

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *