HARAMBEE STARLETS WALIPWA MARUPURUPU YAO BAADA YA MVUTANO
Serikali imetekeleza ahadi yake ya kulipa marupurupu yaliyokuwa yanadaiwa na Harambee Starlets, pamoja na kutoa zawadi ya fedha kama alivyoahidi Rais William Ruto.
Katibu Mkuu wa Idara ya Michezo Elijah Mwangi amesema serikali imetoa Shilingi milioni 10 kama zawadi kwa kikosi hicho na Shilingi milioni 10 nyingine kulipa marupurupu yao.
Hatua hiyo imefuatia siku yenye mvutano ambapo wachezaji wa Harambee Starlets walifika katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) wakitaka kulipwa marupurupu yao kabla ya kuondoka kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON).
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

