OWALO AZINDUA CHAMA KIPYA CHA KISIASA
Aliyekuwa Waziri wa Habari na Teknolojia, Eliud Owalo, amezindua chama kipya cha kisiasa kitakachojulikana kama People’s Prosperity Party, akisema atakitumia kuwania urais katika uchaguzi ujao.
Owalo amesema kipaumbele chake kikuu kitakuwa kuimarisha uchumi na kuboresha maisha ya wananchi iwapo atachaguliwa kuwa rais.
Aidha, amezisuta serikali zilizopita kwa kushindwa kutatua changamoto zinazowakabili Wakenya na kuahidi kutoa mwelekeo mpya wa maendeleo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

