Monday, October 5, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

IEBC YAPENDEKEZA KIWANGO KIPYA CHA  FEDHA ZA MATUMIZI YA KAMPENI

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imependekeza viwango vipya vya juu vya matumizi ya fedha za kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Kwa mujibu wa rasimu hiyo, mgombea urais ataruhusiwa kutumia hadi shilingi bilioni 4.4, huku vyama vya kisiasa vikipewa kikomo cha matumizi ya takriban shilingi bilioni 17.7 wakati wa kampeni.

IEBC imesema mapendekezo hayo yanalenga kudhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi na kuhakikisha ushindani wa haki kwa wagombea na vyama vya kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *