BEI ZA MAFUTA KUPANDA KUANZIA LEO USIKU
Wakenya huenda wakaanza kukabiliwa na ongezeko la bei za mafuta katika miezi kadhaa ijayo baada ya serikali kuonya kwamba vita vinavyoendelea kwenye maeneo ya mashariki ya kati baina ya marekani na Iran vimeanza kupandisha bei za mafuta ghafi duniani.
Katika taarifa kwa umma Waziri wa kawi na petroli Opiyo Wandayi amesema hali hiyo huenda ikaathiri makadirio ya bei za mafuta nchini kuanzia leo huku akiwahakikishia wakenya kwamba hakuna upungufu wa mafuta nchini na kwamba mfumo wa biashara kati ya serikali na serikali yaani G to G umeendelea kuwezesha usambazaji wa mafuta unaoendelea bila usumbufu.
Haya yanajiri wakati ambapo mamlaka ya kudhibiti bei za mafuta na petroli EPRA zinasubiriwa kutangaza bei za mafuta leo hii ili kuanza kutumika kuanzia usiku wa manane.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

