ALIYEKUWA AFISA WA KDF AFUNGWA MAISHA JELA KWA MAUAJI YA MKE NA WATOTO WAKE
Mahakama Kuu imemhukumu aliyekuwa afisa wa KDF Peter Mwaura Mugure, kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya mkewe aliyekuwa ametengana naye pamoja na watoto wao wawili yaliyotokea mwaka 2019.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Martin Muya, ambaye alieleza kuwa kitendo hicho kilikuwa cha kinyama na kubainisha kuwa mshtakiwa hakuonyesha majuto yoyote wakati wote wa kesi.
Jaji amesema adhabu hiyo inalenga kukabiliana vikali na ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake na watoto nchini pamoja na kuimarisha haki kwa waathiriwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

