Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

IEBC YAONYA WAPIGA KURA DHIDI YA KUKIUKA KANUNI ZA UCHAGUZI OLKALAU

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewaonya wapiga kura wa Ol Kalou dhidi ya kupiga picha au kusambaza picha za karatasi za kura zilizokwisha kupigwa alama wakati wa uchaguzi mdogo wa eneo hilo.

Tume hiyo imesema kitendo cha kupiga picha ya kura au kuisambaza ni ukiukaji wa sheria za uchaguzi na kinaweza kuhatarisha usiri wa kura pamoja na uadilifu wa mchakato wa uchaguzi.

IEBC imewataka wapiga kura kuzingatia taratibu za uchaguzi, kulinda siri ya kura zao na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha hatua za kisheria. Aidha, tume hiyo imewahimiza wananchi kujitokeza kwa amani na kushiriki katika uchaguzi kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *