USWISI YATINGA ROBO FAINALI KWA PENALTI
Uswisi imefuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa Colombia 4-3 kwa mikwaju ya penalti, kufuatia sare tasa katika muda wa kawaida.
Kipa Gregor Kobel aliibuka shujaa kwa kuokoa penalti muhimu, kabla ya Ruben Vargas kufunga mkwaju wa ushindi na kuipeleka Uswisi hatua ya robo fainali.
Kwa ushindi huo, Uswisi sasa itamenyana na mabingwa watetezi Argentina katika robo fainali ya Kombe la Dunia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

