MOTO ULIOZUKA SOUTHLANDS LANG’ATA WADHIBITIWA, HAKUNA VIFO
Vikosi vya dharura vimefanikiwa kudhibiti moto mkubwa uliotokea katika eneo la Southlands, Lang’ata jijini Nairobi.
Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limesema hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika mkasa huo, huku juhudi zikielekezwa sasa kutathmini kiwango cha uharibifu uliosababishwa.
Moto huo ulizua taharuki baada ya moshi mnene kuonekana ukifunika anga, na kusababisha vikosi mbalimbali vya dharura kushirikiana kuuzima na kuzuia usienee zaidi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

