Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RYAN OGAM AJIUNGA NA RFC LIÈGE KWA MKOPO

Mshambulizi wa Harambee Stars, Ryan Ogam, amejiunga na klabu ya RFC Liège ya Ubelgiji kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Wolfsberger AC ya Austria.

RFC Liège, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Ubelgiji, inatarajia mabao ya Ogam yataisaidia kupanda hadi Ligi Kuu katika msimu wa 2026/27.

Kwa Ogam, uhamisho huo unampa fursa mpya ya kufufua kiwango chake baada ya msimu wa kwanza uliokuwa na changamoto nchini Austria kufuatia kuondoka kwake kutoka Tusker FC mwaka uliopita.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *