Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

HINGA AWAHIMIZA WAKENYA KUTUMA MAOMBI YA NYUMBA ZA BEI NAFUU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nyumba, Charles Hinga, amewahimiza Wakenya wanaokidhi vigezo kutuma maombi ya nyumba za bei nafuu kupitia jukwaa rasmi la Boma Yangu.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya miundombinu ya mijini pamoja na maafisa wengine wa serikali, Hinga amesema nyumba nyingi tayari ziko tayari kukaliwa katika kaunti mbalimbali nchini.

Amesema serikali inalenga kuongeza umiliki wa nyumba miongoni mwa Wakenya huku ikiendelea kuzalisha maelfu ya nafasi za ajira kupitia miradi ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Imetayarishwa na Cyrus SIfuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *