SIFUNA: LINDA MWANANCHI HAIFADHILIWI NA UHURU KENYATTA
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amekanusha madai kwamba Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anafadhili shughuli za vuguvugu la Linda Mwananchi.
Sifuna amesema shughuli za vuguvugu hilo zinafadhiliwa na wananchi wa kawaida, baadhi ya wabunge na wafadhili wengine, huku akisisitiza kuwa matumizi yake yanaweza kufuatiliwa kupitia kumbukumbu za umma.
Aidha, amesema dhana kwamba wanasiasa lazima wagawe fedha katika mikutano ya hadhara imechangia kuibuka kwa madai kuwa shughuli za upinzani hufadhiliwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

