OMANYALA AONGOZA JEDWALI LA DIAMOND LEAGUE
Mwanariadha wa Kenya Ferdinand Omanyala ameendelea kushikilia nafasi ya juu kwenye msimamo wa mbio za mita 100 za Diamond League, licha ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika mashindano mawili yaliyopita.
Omanyala alimaliza katika nafasi ya sita mjini Paris na ya nane mjini Rome, lakini mwanzo wake mzuri wa msimu umeendelea kumuweka kileleni mwa jedwali la mbio hizo.
Msimamo huo unampa matumaini ya kufuzu fainali za Diamond League zitakazofanyika mwezi Septemba mjini Brussels, Ubelgiji, huku akilenga kurejea katika kiwango chake bora katika mashindano yajayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

