WABUNGE WATAKA MAGEUZI YA HARAKA KUHUSU USALAMA WA SHULE
Wabunge wameitaka serikali kufanya mapitio ya haraka ya sera za nidhamu na usalama shuleni kufuatia ongezeko la visa vya moto katika shule mbalimbali nchini.
Mjadala huo uliibuliwa na Mbunge wa West Mugirango, Stephen Mogaka, aliyeomba taarifa kuhusu utayari wa shule kukabiliana na majanga, uzingatiaji wa kanuni za usalama na viwango vinavyopaswa kutekelezwa ili kuzuia majanga yajayo.
Wakati wa mjadala huo, wabunge walieleza wasiwasi kuhusu kuzorota kwa nidhamu shuleni, wakidai baadhi ya wazazi wameacha jukumu la malezi na kuwaachia walimu pekee wajibu wa kuwaongoza na kuwalea watoto.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

