RAIS WILLIAM RUTO ANG’AA KATIKA UTAFITI WA INFORTRAK KWA ASILIMIA 32
Rais William Ruto angeibuka mushindi wa uchaguzi wa urais iwapo uchaguzi huo ungefanyika hii leo.
Kulingana na utafiti wa shirika la utafiti Infor Track Rais Ruto anaongoza kwa asilimia 32 huku kiongozi wa chama cha WIPER Kalonzo Musyoka akishikilia nafasi ya pili kwa asilimia 13.
Aidha aliyekuwa naibu wa Rais Rigadhi Gachagua na aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang wanafutana kwa asilimia 12 kila mmoja, utafiti huo pia umebainisha kuwa asilimia 13 ya waliohojiwa bado hawaja amua mgombea watakaye muunga mkono jambo linaloonyesha kuwa kundi hilo linaweza kuwa na ushawishi mkubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

